
Waziri wa fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba amesimama Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho yatakayofanyika na kuanza kutumika kuanzia October 1, 2022.
Marekebisho aliyoyataja ni pamoja na kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa Benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000
Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.
1. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya
simu (pande zote).
2. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.
3. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki
nyingine.
4. Wafanyabiashara wadogo hawatahusishwa kama ilivyo kwenye
kanuni za sasa.
5. Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia
wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi
30,000.
6. Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50
kufuatana na kundi la miamala. Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo
viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu
cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000.
0 Comments