Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam
Ikiwa ni siku chache kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii, wachezaji wa Timu ya Yanga wametoa ujumbe mahsusi wakihamasisha wapenda michezo na watanzania wote kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la kitaifa la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kuanza rasmi mnamo tarehe 23 August 2022.
Kutokea Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es salaam, Mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara wametoa salamu zao kwa wapenda michezo kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii siku ya Jumamosi.
#Sensabika ndio kauli inayovuma kwa kasi zaidi kwa kipindi hiki ikiwa ni sanjari na kupongeza juhudi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Zoezi la Sensa ni kati ya mambo muhimu yanayofanywa kwa malengo ya kukusanya taarifa za wananchi ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo nchini.
Wachezaji hao walio katika maandalizi ya mtanange wa siku ya Jumamosi wametumia saa kadhaa kutoa ujumbe wa kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la kitaifa la Sensa ya watu na makazi.
Zoezi la Sensa linafanywa na serikali ikiwa ni sehemu ya mipango ya Kisera inayolenga kuboresha huduma za jamii na mipango mingine endelevu ya kimaendeleo. #Sensabika ndio mpango mzima kwa wanamichezo na wapenda maendeleo wote.
Cheza Video Hapa Chini 👇🏻
0 Comments