HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TLS IMESIMAMA YENYEWE BILA NGUZO YA WANACHAMA

  Na AMEDEUS SOMI,

DSM,

Mgombea Urais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Prof.Edward Gamaya Hoseah amesema kwa kupitia kipindi cha uongozi wake amewezesha Chama hicho kujiendesha chenyewe pasipo kutegemea michango ya wanachama.

Ameyasema hayo wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa tena katika kipindi kingine cha awamu ya nafasi hiyo.




           Mgombea Urais TLS  Prof. Edward Gamaya Hoseah     

“Wanachama wa TLS wana imani kubwa na mimi tangu nilipoingia kwenye uongozi Mwezi May mwaka jana, na asilimia kubwa ya masuala ambayo niliwaahidi tumeyatimiza kwa ufanisi”

“Mimi nimefanya kazi na serikali, najua namna bora ya kushirikiana na serikali kwa manufaa ya TLS bila kuathiri uendaji kazi wake kama taasisi na ndiyo maana nimekuja na sera ya kujenga ama kwa kiingereza ‘Constructive engagement’. “

“ Kuna pesa ambayo ilipaswa kurejeshwa na mahakama, ambayo ni pesa halali ya mawakili tangu Mwaka 1954 marejesho hayakuwahi kufanywa, lakini hivi karibuni tumezungumza na mahakama kuangalia namna ya kuzirejesha. Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 TLS inatarajia kupokea Tshs. Milioni 450 kutoka hazina.” 

“Kipindi cha UVIKO19 tulipoteza baadhi ya Mawakili, kwa sababu gharama za bima zilikua kubwa, na nilipoingia madarakani nilikikuta hicho kilio na kukifanyia kazi kwa kuhakikisha gharama ya bima ya Afya inashuka kwa wanachama wa TLS kutoka shilingi Milioni 1.5 mpaka laki 5 pekee”

“Gharama za kulipia leseni kwa Mawakili zilikua kubwa, hii iliepelekea Mawakili hasa vijana kulalamika kulipa  kiasi cha shilingi 240,000, kama kiongozi niliwasikia kilio chao na tumefanikiwa kushusha kiwango cha ada husika mpaka kufikia Shilingi 120,000.”






Post a Comment

0 Comments