HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HIVI NDIO VIPAUMBELE KUMI KWA MGOMBEA URAIS WA TLS EDWARD HOSEAH

 Na AMEDEUS SOMI,
Dar es Salaam,

Mgombea kiti cha Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Prof.Edward Gamaya Hoseah ametoa mapendekezo kumi atakayoyaendeleza katika kipindi kingine cha uongozi wake endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.


Hivi ndivyo vipaumbele alivyojinadi Prof. Hoseah ambaye ni msomi pia wa mambo mbalimbali ikiwemo Uongozi


                Prof.Edward Hoseah Mgombea Urais TLS



1. Kuitegemeza TLS kiuchumi na kuepuka kutegemea michango ya wanachama kujiendesha. 


-Mahitaji ya uendeshaji wa TLS ni takribani Shilingi Bilioni 6 huku michango ya wanachama ikifikia Shilingi Milioni 600 pekee.


2. Kuhakikisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha TLS kinafanya kazi kwa ufanisi ili kusaidia wanachama wenye uhitaji na huduma.


3. Kuimarisha zaidi utoaji msaada wa kisheria kwa wananchi hususani wasiokuwa na uwezo wa kifedha. Ili kufanya jambo hili liwe endelevu tutashirikisha Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha kunakuwepo ofisi za kudumu.


4. Kuimarisha Taasisi ya kitaaluma (Professional enhancement Institute) itakayoweza kuongeza weledi kwa Mawakili na kuwawezesha kufanya vizuri zaidi kimataifa.


5. Kuihusisha serikali kwenye mambo mbalimbali ya kujenga ili kuimarisha mifumo ya utoaji haki nchini na kuwawezesha Mawakili kufanya kazi zao kwa ufanisi.


6. Kuhakikisha kituo cha Utatuzi wa Migogoro ya kibiashara (Tanzania International Arbitration Centre) kinajengwa na kufanya kazi nchini kwa ufanisi.


7. Kuendeleza shughuli za uwekezaji ndani ya TLS kwa mujibu wa taratibu za TLS. 


8. Kamati za Tanganyika Law Society zitazingatia swala la kijinsia. Kama tulivyoonyesha katika uongozi wa mwaka mmoja uliopita, tutaendelea kutekeleza mipango jumuishi inayolenga kuleta usawa wa kijinsia ili kutoa nafasi sawa kwa makundi yote katika jamii.


9. Kuwapa fursa mawakili vijana. Katika mwaka mmoja tumefanikiwa kupunguza gharama za ada kwa Mawakili na kutoa nafasi mbalimbali kwa vijana, ajenda hii itaendelea kutekelezwa kwa kutoa nafasi kwa Mawakili vijana na kutatua changamoto zinazowakabili.


10. Kuwapa kiupambele wanachama wenye mahitaji maalumu. Dhana jumuishi itaendelea kuwa kipaumbele ili kuleta usawa kwa Mawakili wenye mahitaji maalum.

Post a Comment

0 Comments