Na AMEDEUS SOMI,
Dar es Salaam,
Mgombea Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Prof.Edward Hoseah ameahidi na kuja na vipaumbele vifuatavyo
1. HUDUMA NA USTAWI WA WANACHAMA
- Mpango wa Bima nafuu kutoka TZS 1,056,000 mpaka kufikia TZS 500,000 kwa mwanachama kwa mwaka.
-Juhudi za kufanya mazungumzo na Mahakama kuhakikisha miundombinu rafiki kwa Mawakili wenye ulemavu katika majengo ya mahakama.
- Kuwezesha jukwaa la Mawakili Vijana
- Kushusha tozo na ada ya Mawakili kutoka TZS 60,000 hadi TZS 20,000
- Kuandaa warsha na makongamano mbalimbali kwaajili ya kuwajengea uwezo Mawakili.
PROF EDWARD HOSEA KATIKA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA 2021-2022
KATIKA UTAWALA WA SHERIA, HAKI NA UTU
Aidha Prof.Hosea ameendelea kujinadi na sera mbalimbali ikiwemo haki na misaada ya kisheria kwa wanachama kama ailivyoainisha.
1. Tumeweza kuboresha Huduma za Msaada wa Kisheria kwa kufanya yafuatayo
2. Tumepanua wigo wa utoaji wa msaada wa kisheria kutoka kuwa zoezi la wiki moja mpaka kuwa zoezi la kudumu.
3. Tumefanikiwa kushawishi serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kutoa ruzuku ya TZS 1.2 bilioni kwa TLS kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.
4. Tumefanikiwa kushiriki katika mashauri mbalimbali chini ya mpango wetu wa huduma za msaada wa kisheria na chini ya mpango wa mashauri yenye maslahi ya umma.
0 Comments