Na Mwandishi Wetu,
Ikiwa zimebaki siku chache tu kufungwa mchakato wa uchukuaji fomu ya kuwania Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro Joseph Tadayo jana January 13, 2022 amechukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema amechukua fomu kugombea nafasi hiyo kutokana kuwa na sifa zinazotakiwa.
"Leo nimefika kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania"
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Msaidizi idara ya Oganaizesheni, Bw. Solomon Itunda amesema jumla ya wanachama 49 wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo mpaka jana Alhamisi Januari 13, 2022.
Aidha Bwana. Itunda amewataka wanachama wote ambao wamechukua fomu kutumia siku mbili hizi kati ya kesho na kesho kutwa kukamilisha mchakato huo na kuwatoa wasiwasi kuwa kiwa na imani kwani haki itatendeka na anayestahiki atapewa.
0 Comments