Na AMEDEUS SOMI,DSM
Serikali kupitia Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta.
Taarifa iliyotolewa leo na EWURA inaeleza kwamba, Ikilinganishwa na bei za mwezi Desema 2021, bei za Januari 2022 zitapungua kwa kati ya Shilingi 4 na 35 kwa lita ya petroli; na kati ya Shilingi 43 na 67 kwa lita ya dizeli isipokuwa kwa bandari ya Mtwara ambapo bei zitaongezeka kwa Shilingi 2 kwa lita; huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Shilingi 99 kwa lita.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika oisi za EWURA, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godrey Chibulunje amesema
Moja kati ya hatua muhimu zilizosababisha kushuka kwa bei hizo, ni kupunguzwa kwa tozo za taasisi za Serikali.
Vilevile, kutokana na kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, Serikali iliahirisha ukusanyaji wa ada ya mafuta (petroleum fee) kuanzia Desemba 2021 na hivyo kufanya bei ya juu kufikiwa katika mwaka 2021 kuwa ni Shilingi 2,510 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam, Shilingi 2,525 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Tanga na Shilingi 2,569 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.
Bila ya kufanya maamuzi haya, bei za mafuta zingefikia kiwango cha juu cha Shilingi 2,638 kwa lita ya petroli (Dar es Salaam), Shilingi 2,648 kwa lita ya petroli (Tanga); na Shilingi 2,693 kwa lita ya petroli (Mtwara).
KUHUSU MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA NCHINI
Bei za mafuta hukokotolewa kwa kutumia Kanunu za Ukokotoaji za bei za mafuta-EWURA (Petroleum Products Prices Setting) Sheria ya mwaka 2009 na uundwaji wa kanunu hizi huzingatia maoni ya wadau mbali kabla ya kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.
Kanunu hiyo imeainisha gharama mbalimbali za lazima katika biashara ya mafuta. Gharama hizo ni pamoja na gharama za mafuta (FOB prices), gharama za uagizaji (Premium),gharama za uendeshaji wa biashara kwa jumla na rejareja (Wholesale and Retail Margins) tozo na ada za taasisi mbalimbali za serikali, kodi na gharama za usafirishaji
0 Comments