Na AMEDEUS SOMI
MABINGWA wa watetezi wa ligi kuu Simba, wakiwa ugenini leo Octoba mosi, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo uliochezwa kwenye dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.
Dodoma Jiji walionekana kukamia mchezo huo kutokana na wachezaji wao kutumia nguvu kubwa kukabiliana na wachezaji wa Simba hali iliowafanya kucheza rafu za mara kwa mara.
Matumizi hayo ya nguvu yalipelekea mchezaji Anuary Jabir kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Kennedy Juma, ambaye alitoka baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.
Muuaji wa Dodoma Jiji alikuwa Meddie Kagere aliwafunga bao dakika ya 70 ya mchezo akipokea pasi safi ya kichwa kutoka kwa Chris Mugalu.
Simba ililazimika kufanya mabadiliko ya lazima baada ya wachezaji wake watatu kuumia Sakho, Kennedy Juma na Tadeo Lwanga, kwa matokeo hayo sasa Wekundu wa msimbazi wamefikisha alama 4 baada ya kushuka dimbani mara mbili.
0 Comments