Na AMEDEUS SOMI
Mmilili wa Makampuni ya Mitandao ya kijamii ya Whats App, Facebook na Instagram Bwana Mark Zuckerberg ameibuka hadharani na kuwaomba radhi watumiaji wa mitandao hiyo duniani kwa kile kilichotokea siku ya jana ambapo mitandao hiyo haikuwa hewani kwa muda wa saa zaidi ya sita (6)
Kwa mujibu wa tovuti ya walesonline.co.uk imesema bwana Mark amesema hawakudukuliwa bali ni mabadiliko mabaya na ya ghafla ya kimifumo "faulty configuration change" nadir iliyopelekea huduma hizo kutoweka hewani.
Nyinginezo
https://somisports.blogspot.com/2021/10/simba-sc-yaikalisha-dodoma-jiji-jamhuri.html
https://somisports.blogspot.com/2020/11/majeraha-yanavyowaharibia-mipango.html
Mbali na hilo Mkurugenzi huyo alisema waliwataarifu watumiaji wake kea kupitia ukurasa rasmi wa twitter kwa kusema "Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza lakini timu yetu ya mafundi ipo kazini kuhakikisha tunatatua tatizo hili haraka iwezekanavyo"
Aisha Mkurugenzi huyo ambae pia ndio mwanzilishi wa Facebook amesema kwa tukio tu la jana limemsababishia hasara ya zaidi ya dola 6.1 Billioni . hata hivyo amesema watajitahidi kuhakikisha adhari hiyo haitajitokeza tena kwa sababu anaamini jamii na kundi kubwa la watu linawategemea wao katika kuendesha shuhuli zao.
Kwa sasa huduma hiyo imesharejea na watumiaji wanaendelea kutumia kama kawaida lakini kingine ambacho ulikuwa hujui ni kwamba kampuni ya Twitter imeongeza idadi ya watumiaji 59.6 Millioni kitendo kile cha jana.
Endelea kuwa karibu nasi tukuhabarishe na kukuelimisha.
0 Comments