HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MAHARUSI GHANA WAVUNJA REKODI YA KEKI KUBWA MITHILI YA GARI AINA YA V8

Na AMEDEUS SOMI


Video inayowaonyesha maharusi nchini Ghana Derrick na Sandra wakiwa katika hisia za kimapenzi ndani ya keki kubwa iliyotengenezwa kwa ukubwa wa gari aina ya PRADO V8 imezua kitete mitandaoni.

Video za harusi yao zilianza kusambaa kwa kazi na kuzua hali ya kushangaza wengi katika mitandao nchini Ghana.Bwana mmoja aitwaye Kwaku yeye alikuwa Mubashara katika ukurasa wake wa Instagram akionyesha tukio hilo.

Bwanaharusi ndiye aliyekuwa wa kwanza  kufungua milango ya gari hiyo (garicake) akishikilia kwa nguvu matairi  kisha kufungua milango na kuanza kupanda yeye na mkewe ambaye ni bibi harusi wageni waliokuwa pale pamoja na wanafamilia wakianza nderemo na vifijo vya kutosha mno.

Keki hiyo inakadiriwa kuwa ya gharama zaidi duniani kwani ingawa mbunifu wa Cake hii Bw. Joe hakutaka kuweka wazi lakini kwa wataalam wa hizi kazi kutokea hapo Ghana wanasema inakadiriwa kufikia Cedis 50.000 (Pesa ya Ghana) Ambapo ukiigeuza kwa fedha za Tanzania ni sawa na Shilingi Milioni 18,1999,158.42.

Pamoja na vitu mbalimbali vilivyosheheni kwenye Cake hiyo ina uzito wa Kg.200 na imemgharimu mwezi mzima kuitengeneza.

Kama unajiona wewe ni mbunifu uliyepitiliza hapa kuna somo la kujifunza dunia ni kubwa mno hatuwezi kuijaza.

Je? Unaweza kununua Cake ya Milioni 18?.... Au unaweza kuvumilia kusubiri Cake kwa muda wa mwezi mzima? au utachukua tu zile za Makumbusho ambazo unatoa oda leo, kesho umeshapewa tena kwa bei chee tu Elfu 40....?




 

Post a Comment

0 Comments