HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RONALDO ASHINDWA KUIBEBA JUVENTUS IKITUPWA NJE UEFA

Ronaldo ana Gundu? Binadamu! Muogope sana binadamu anapokuwa katika kilele chake cha ubora wa kufikiri, anaweza kuwa binadamu wa aina nyingine kabisa mbele ya binadamu wenzake.

Binadamu hupishana hapa tu. Fikra!! Fikra zinaishi. Katika wale binadamu 44 ambao wamekufa lakini bado dunia bado inaamini kuwa bado wanaishi huwezi kukosa kulitaja jina la Adolph HittlerBado anaishi huyu.
Miongoni mwa sheria zake za kijeshi alizokuwa akizitumiaa wakati huo ndizo ambazo mataifa mengi huzitumia leo hii. Hayupo Adolph Hitler lakini fikra zake zinaishi.

Umewahi kumsikia Leopald Sedar Senghor? Hujawahi. Na huenda likawa jina geni kabisa masikioni mwako. Huyu ni raisi wa kwanza Senegal.

 Senghor ni miongoni mwa waafrika wachache waliopo katika orodha ile ya watu 44 ambao dunia bado inaamini uwepo wao. Bado anaishi Senghor unajua kivipi? Ni mwafrika wa kwanza kuandika juu ya mwafrika, kuandika kila kitu kuhusu mwafrika. Haitoshi.

 Ni mwafrika pekee aliyeshiriki katika kutengeneza lugha ya kifaransa. Senghor Bado anaishi kwa peni yake na fikra zake dunia itaendelea kumkumbuka milele. 
Kumtazama Ronaldo katika ubora wake ilikuwa haitofautiani sana na kumtazama Priyanka Chopra akiwa katika vazi lake la kulalia. Kaka yangu Idrisa Shomary yeye ni shabiki wa Messi lakini aliwahi kuniambia kuwa alikuwa akiwahi kwenda kwenye mabanda ya video kumtazama Ronaldo akipasha misuli yake moto achilia mbali kucheza uwanjani ni hivyo hivyo kwa Roberto Carlos naye alikaririwa na waandishi wa habari kuwa alikuwa akiwahi kwenda uwanjani kwa ajili ya kumtazama Ronaldo akipasha.

 Baada ya Klabu ya Juventus kushindwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Klabu bingwa Ulaya kwa Mara ya 3 Mfululizo kuna minong’ono imeanza kuibuka ya kwamba ni kama Supastaa wa Klabu hiyo Cristiano Ronaldo kuja na gundu. Mwaka Mmoja kabla ya Ronaldo kusajiliwa Juventus walifanikiwa kutinga hatua ya Fainali Msimu wa 2016-17. 

Ndani ya Miaka Minne kabla ya CR7 kutua kwa Vibibi Vizee hao wa Turin. Juventus waliingia Fainali ya Uefa mara Mbili (2016-17 na (2014-15). Hii ni Mara ya Kwanza kwa CR7 kushindwa kuingia Hatua ya Robo Fainali ya Uefa kwa Misimu Minne Mfululizo.

 Katika msimu wa kwanza wa Ronaldo akiwa na jezi ya kibibi kizee walitolewa na Ajax kwenye robo fainali kwa jumla ya mabao 3-2. Msimu uliopita Juventus walitolewa na Lyon kutoka raundi ya 16 bora baada ya mchezo kumalizika 2-2 huku Lyon wakisonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini.Msimu huu ndio kama mlivyosikia wamesukumizwa nje tena kwa sheria ile ile iliyowahukumu misimu iliyopita. Kwa mantiki hiyo ni kweli usajili wa Kiumbe huyu mwenye kipaji cha kipekee kutoka Funchal Ureno hauna tija?

. Licha ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu duniani bado haikuweza kuisaidia Bianconeri kuvuka katika hatua hiyo ngumu. Yaweza kuchukuliwa kimasihara lakini Cr7 ni mshindi wa tuzo ya Ballon D’or kwa mara tano nyuma ya Lionel Messi La Pulga.

 Ni kweli takwimu zinambeba Ronaldo kwani uhodarin wake wa kuchana nyavu ndio uliompa vikombe vitano vya UEFA akiwa na Real Madrid pamoja na Mashetani wekundu Manchester United. Mashabiki wa Juventus ndani ya uwanja wao jijni Turin walijikuta wakiviacha viti vyao na kuinuka kumshangilia Ronaldo.
 Ni ngumu sana lakini kwa ubora na bao alilowafunga ilibidi tu mashabiki wa Juventus kumshangilia mchezaji wa Real Madrid tena katika uwanja wao wa nyumbani. Wazungu sio wanafki. Dunia itawezaje kumsahau huyu mtu? Ataishi tu, hata baada ya kizazi chetu kupita. Wapo baadhi ya waandishi na magazeti mbali mbali yameandikia kuhusu Ronaldo kushindwa kuisaidia Juve kupenya katika robo fainali , ikiwemo Ronaldo kugeuka kwenye ukuta wakati mpira wa faulo ya mwisho ya Sergio Oliveira kumshinda Szczesny na kutinga wavuni. Kimsingi unaweza kufanya mengi mazuri kwa wakati fulani lakini kwa muda mfupi tu ukasahaulika hata kwa uliyofanya, kwa kisa tu cha eti sisi ni binadamu, tuna hulka ya usaahulifu.

 Ukweli ni kwamba kwa aliyofanya Ronaldo ni ya kuheshimika na ataishi tu. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee kwani amebakisha miaka miwili katika kandarasi yake ambayo inatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments