Na Amedeus Somi,
Sijui ni upepo wa aina gani unaozikumba timu mbalimbali barani Ulaya na duniani kwa kipindi cha hivi karibuni.Ni vyema zaidi kusema kwamba ni kama nuksi au kuchoka kwa baadhi ya wachezaji waliotumika mno katika vilabu vyao ndio kinachopelekea kupata pancha.
Ni ukweli usiopingika kuwa majeraha hayaepukiki katika soka au mchezo wowote unaohusisha kukabana kwa kukaribiana au hata mara nyingine yaweza kutokea mchezaji akiwa peke yake pasipo kuguswa anaweza kujitengenezea majeraha.
Ndio hali ilivyo kwa sasa kwa baadhi ya wachezaji wa vilabu vikubwa barani Ulaya, hasa zaidi katika zile ligi kubwa 'Big Five' ikiongozwa na ile ligi pendwa ya EPL ya pale kwa Malkia.
Majeraha jumlisha na Kale Kahandsomeboy ka Wuhan wanakiita Covid-19 ndio umekuwa wimbo unaoimbwa kichwani mwa makocha wengi mara tu vinapowafika nyota wao.
Ukiachilia mbali ile ya Blaise Matuidi na Muargentina Paul Dyabala ambao ndio moja kati ya wachezaji wa kwanza kwanza kukumbwa na Covid. Kuna rundo la wachezaji wengi ambao waneshindwa kuendelea kupambania Klabu zao kwa matatizo kama hayo au majeruhi ya muda mrefu na mfupi.
PARIS SAINT GERMAIN
Tukianza na Matajiri wa jiji la Maraha Paris, Paris Saint Germain wao unaambiwa ni kijiji kama sio wachezaji asilimia 95 wa kikosi cha kwanza wote wakikumbwa na majeruhi.
Ukizingatia hawakuanza ligi vizuri bado kile kijini majeraha kimetanda kwao kwani wachezaji wafuatao ndio watakao kaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma na wengine miezi kadhaa.
Majeruhi Waliopo
1.Juan Bernat-Goti aliumia katika mechi kati ya PSG dhidi ya Metz akitolwa nje kwa kushindwa kuendelea. Kwa sasa Bernat ameshaanza mazoezi mepesi.
2.Neymar-Aliumia msuli wa nyuma wa paja (Hamstring) katika mchezo wa makundi ya Uefa Champions League dhidi ya Istanbul Basaksehir ndani ya dakika 26 pekee na nafasi yake ikachukuliwa na Pablo Sarabia kurejea kwake ni Nov 13.
3.Presnel Kimpembe-ameanza mazoezi mepesi hivi karibuni alikuwa akiuguza jeraha la mguu
4.Keylor Navas-Matatizo ya Misuli lakini ameanza mazoezi mepesi.
5.Mauro Icardi-goti
6.Marco Veratti-
7.Julian Draxler-
8.Pablo Sarabia-
9.Idrissa Gana Gueye-
10. Moise Kean-
11.Alesandro Florenzi na
12.Thilo Kehrer
LIVERPOOL VIJOGOO
Ukuta Wote wa Liverpool sasa umedondoshwa na mchwa
1.Vijl Van Dijk
Kwa upande wa Liverpool mi dhahiri sasa Ukuta wote umebomoka kama tetemeko la ardhi kwa sababu ya majeruhi...wanasema mapango sio matumzi. Achilia mbali Vijl Van Dijk aliyegongana na kipa wa Everton katika ile derby ya Liverpool yeye usimwesabie mwaka huu laaah hasha yeye ni kwamba shuhgili yake imeisha unaambiwa hadi mwakaniiii
2.Trent Alexander Anold
Haya ukija kwa beki wa pembeni mwingereza Trent Alexander Anold naye ni kitandani baada ya kuumia katika mchezo wa man City.
3.Fabinho
Fabinho yeye aliumia misuli ya nyuma ya paja katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Midtjylland.
4.Joe Gomez
Joe Gomez aliumia goti la mguu w a,ushoto na tayari ameshafanyiwa upasuaji ambapo ilionekana baadhi ya mifupa ina shida na sasa imesharekebishwa.
5.Mohamed Salah
Mohamed Salah yeye alibainika kukutwa na homa ya virusi ya Corona Ijumaa iliyopita ya tarehe 13 wakati timu yake ya Taifa Misri ikijiandaa ucheza na Togo katika michuano ya kufuzu Afcon 2022.
Straika wa Liverpool Mohammed Salah ambaye amekutwa na Corona |
6.Jordan Henderson
Jordan Henderson alitolewa katika mchezo wa timu yake ya Taifa ya Uingereza wakati ikipokea kipigo cha magoli 2-0.
7.Andy Robertson
Na wa mwisho katika ule ukuta wa Liverpool ambaye kwa sasa yupo ama sebuleni kwake anaugulia maumivu au wodini hospitali ni Andy Robertson raia wa Scotland akiwemo kwenye kikosi kilichoitoa Serbia kwa mikwaju ya Penalti na Andy Robertson alicheza kwa adaikiaka zote 120.
Majeruhi Wengine
Pancha nyingine mpya ni Hii ya Sergio Ramos akiumia katika ushindi mnono wa Hispania kuwanyoosha Ujerumani kwa mabao 6-0 huku ikisemekana hata hivyo jeraha lake ni dogo. Ila anakweda kumweka Zidane hati hati kwani beki wa Ufaransa Rafael Varane naye aliumia katika mechi za Kimataifa za weekend hi.
Hali hii ya Majeruhi jumlisha Covid kwa upande mwingine ni neema kwa timu nyingine abazo pia hazikwa na Nature ya kupagawishwa na kelele za majukwaani.
Mfano wa Klabu hizo ni kama Leicester City ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote wa Ligi ya Premia.Ikiwa imecheza michezo 8,ikishinda 6 na kudroo miwili.Kwa sasa wanaonekana wamepania kuutaka ubingwa kwani inaonekana tayari wamejifunza au wamejutia yaliyowakuta kabla na baada ya msimu uliopita kwani walikua na nafasi nzuri sana ya kutwaa ama kucheza UEFA na matokeao yake uzembe waliofanya wakajikuta wanamaliza ligi katika nafasi ya 5.
Hadi tunaelekea kwenye break ya kimataifa vijana wa Brendan Rogers ndio wanaongoza ligi wakiwa na pointi 18 wakifatiwa na vijana wa Jose Mourinho wenye 17.
0 Comments